Jumatatu 18 Mei 2026 - 15:11
Kivuli cha mateso ya Kizayuni juu ya Wapalestina katika ukimya wa vyombo vya habari na mazingira ya vita vya Marekani dhidi ya Iran

Hawza/ Wakati dunia kila siku inatangaza habari zinazohusiana na vita vya Marekani na Israel dhidi ya Iran pamoja na mashauriano ya kisiasa ya kikanda na kimataifa, katika kona nyingine ya dunia Wapalestina bado tangu miaka 78 iliyopita hadi leo wanaendelea kuishi chini ya kivuli cha mateso ya Wazayuni juu ya vichwa vyao.

Kwa mujibu wa ripoti ya kitengo cha kimataifa cha Shirika la Habari la Hawza, “Mun‘im”, daktari wa Kipalestina, katika kumbukumbu ya Siku ya Nakba amechapisha ripoti zenye uchungu na maumivu makubwa kuhusu hali ya watu wa Palestina tangu zamani hadi leo.

Mwaka 1948 ni mwaka wa Nakba (mateso); katika mwaka huo, nusu ya wakazi wa Palestina ya kihistoria walifanywa wakimbizi, maelfu ya watu wengine waliuawa na kuchinjwa, na maelfu ya majeruhi wakabaki. Mei 15; siku ambayo Wazayuni waliandika historia kwa uhalifu na makumi ya miji ya kihistoria ya Palestina ikaharibiwa, ni mwaka wa sabini na nane wa janga lililoijeruhi Palestina na Umma wa Kiislamu milele. Wazayuni katika siku hizi waliandika juu ya ukuta wa Msikiti wa Al-Aqsa: “Mateso mengine yapo njiani.” Lakini ukweli ni kwamba mateso kwetu hayajawahi kumalizika; ni sura yake tu ndiyo imebadilika.

Mwaka 1917, wakati ukoloni wa Uingereza ulipoweka mguu wake Palestina, idadi ya Wayahudi waliokuwa wakiishi Palestina ya kihistoria ilikuwa chini ya watu elfu 50, lakini Waingereza kupitia mpango wao mchafu waliwezesha uhamiaji wa Wayahudi kutoka sehemu mbalimbali duniani kwenda Palestina, hadi mwaka 1948, idadi hiyo ilifikia watu elfu 460, yaani ndani ya kipindi kisichozidi miongo mitatu, idadi ya Wayahudi iliongezeka karibu mara kumi, kwa hakika huu haukuwa “uhamiaji”; huu ulikuwa “ubadilishaji wa idadi ya watu” na utayarishaji wa mauaji ya kimbari.

Katika miaka hiyo, Uingereza na nguvu nyingine za kikoloni duniani ziliunda makundi ya kigaidi ya Kizayuni kama Irgun, Haganah na Stern – kwa msaada wa silaha na fedha, makundi haya mwaka 1947 yalianza operesheni ya utakaso wa kikabila, walishambulia miji kama Yafa, Haifa, Safad na Be’er Sheva, wakachoma nyumba moto, wakabomoa kuta juu ya wakazi wake na kuwaua maelfu ya raia wasio na hatia, lakini Wapalestina hawakuruhusiwa kuwa na silaha. Waingereza walikuwa wamewachukulia silaha zote, baba zetu na mababu zetu waliinuka dhidi ya Wazayuni waliokuwa wamejihami hadi meno kwa kutumia majembe, sururu na bunduki rahisi za kuwindia, lakini mbele ya mizinga, vifaru na ndege zilizokuwa zikisaidiwa na Uingereza, hawakuwa na lolote la kusema. Hii haikuwa vita; huu ulikuwa ni utekelezaji wa mauaji ya halaiki chini ya usimamizi wa moja kwa moja wa nguvu za kikoloni.

Kutokana na uhalifu huu, zaidi ya Wapalestina laki saba – yaani nusu ya watu wa Palestina – walifanywa wakimbizi, zaidi ya vijiji na miji ya kihistoria 400 viliharibiwa kabisa au kuachwa bila wakazi, maelfu ya watu waliuawa na kuchinjwa, Taifa moja lilifukuzwa kutoka katika nyumba zake; kwa sababu tu lilikuwa la Kiarabu na la Waislamu, Na leo pia, baada ya miaka 78, Nakba haikumalizika bali inaendelea waziwazi mbele ya macho ya dunia.

Babu yangu alikuwa mkazi wa Yafa, mwaka 1948, wakati makundi ya Kizayuni yaliposhambulia Yafa na kuchoma nyumba moto huku yakiwaua wapendwa wake mbele ya macho yake, hakukuwa na njia nyingine isipokuwa kukimbia, na akawa mkimbizi katika Ukanda wa Ghaza; sehemu ileile ambayo leo tena inageuzwa majivu chini ya mabomu ya itikadi hiyo hiyo ya mauaji ya kimbari, katika miaka yote ya ukimbizi huko Ghaza, babu yangu hakuwahi kuchoka kuizungumzia Yafa, kwa shauku na majonzi yasiyo na mwisho, alikuwa akizungumzia bustani zake za machungwa, mitaa ya mawe ya Yafa, bahari, majirani, na nyumba ambayo ufunguo wake aliuhifadhi kifuani mwake hadi siku ya mwisho ya maisha yake, kila usiku kabla ya kulala alikuwa akisubiri wakati wa kurejea nyumbani kwake, Kila mwaka tarehe 15 Mei, alikuwa akisema: “Huenda mwaka huu…” Lakini wakati huo haukuwahi kufika.

Babu yangu alifariki akiwa uhamishoni bila ya kuikanyaga tena ardhi ya Yafa kwa nyayo zake.

Suala la Palestina baada ya Tufani ya Al-Aqsa; je, tufani nyingine iko njiani?

Operesheni ya Tufani ya Al-Aqsa ilihuisha tena kadhia ya Palestina ambayo ilikuwa karibu kusahaulika duniani, lakini baada ya kupita takribani miaka mitatu na kuwepo kwa usitishaji vita wa juu juu katika Ukanda wa Ghaza, duru za kisiasa na vyombo vya habari kwa uelekezaji wa siri zimekuwa zikilishughulikia kwa kiwango kidogo suala la Palestina, maswali na hofu nyingi kuhusu hatima ya watu wa Ghaza zimebaki bila majibu katika fikra za watu duniani.

Katika vita vya Marekani na Israel dhidi ya Iran, kutokuwepo kwa wazi kwa harakati za mapambano za Palestina sambamba na makundi mengine ya muqawama kumeibua maswali kwa watu; je, makundi ya muqawama ya Palestina yako katika hatua ya kujijenga upya, au hali ya amani inayodaiwa na usitishaji vita dhaifu huko Ghaza imeyafanya makundi ya muqawama kuonekana kana kwamba yamefungwa mikono?

Uvamizi wa nyumba na mashamba ya watu, mateso, mashambulizi ya kinyama na kuvunjiwa heshima Msikiti wa Al-Aqsa kama ilivyokuwa zamani, vinaendelea siku hizi pia chini ya kivuli cha ukimya wa vyombo vya habari na kushughulishwa kwa duru za kisiasa na kimedia na vita vya Marekani na Israel dhidi ya Iran.

Katika siku za hivi karibuni, Wazayuni waporaji kwa kuvamia viwanja vya Msikiti wa Al-Aqsa waliivunjia heshima sehemu hiyo takatifu, na zaidi ya walowezi wa Kizayuni waporaji 1400 chini ya ulinzi wa majeshi ya uvamizi waliingia katika eneo la Msikiti wa Al-Aqsa, katika mikusanyiko hii, kama ilivyo kawaida, heshima ya Msikiti wa Al-Aqsa huvunjwa na Mtume Mtukufu (saww) hutukanwa na watoto wao.

Huko Ghaza, licha ya usitishaji vita unaodaiwa na Wazayuni, wakati wowote wanaotaka wanafanya mauaji na mashambulizi dhidi ya Wapalestina, wakiwemo makamanda, wanawake na watoto wa Ghaza, mauaji ya hivi karibuni ya Izzuddin Al-Haddad, mmoja wa makamanda wa Brigedi za Qassam, yalifanyika katika muktadha huu.

Wakati vyakula na dawa vinapatikana kwa kiwango kidogo sana, maafisa wa afya wa Ghaza wanatahadharisha kuhusu afya na maisha ya wagonjwa wa Ghaza, kwa mujibu wa taarifa za vyanzo vya habari, asilimia 46 ya dawa muhimu, asilimia 66 ya vifaa vya kitabibu na asilimia 84 ya bidhaa zinazohusiana na maabara na benki za damu zimefikia kiwango cha kutokuwa na akiba kabisa. Watoto wa Kipalestina ndio wahanga wakuu wa vita vya Ghaza na kupuuzwa kwa jamii ya kimataifa kuhusu suala la Palestina, Umoja wa Mataifa umetangaza kwamba; tangu mwaka 2025, kwa wastani kila wiki mtoto mmoja wa Kipalestina huuawa kishahidi katika Ukingo wa Magharibi na majeshi ya Kizayuni.

Kivuli cha mateso ya Kizayuni juu ya Wapalestina katika ukimya wa vyombo vya habari na mazingira ya vita vya Marekani dhidi ya Iran

Mashambulizi dhidi ya wanaoswali katika Ukingo wa Magharibi pia ni jambo la kawaida kwa Wazayuni, katika video moja ilioneshwa kuwa askari wa uvamizi mara tatu mfululizo waliwazuia watu kuswali katika kijiji cha Tana mashariki mwa Nablus (Ukingo wa Magharibi).

Mun‘im kuhusu video za ukimbizi wa Wapalestina aliandika: “Nilitaka kuchapisha katika chaneli picha za kumbukumbu za mwaka wa Nakba na uhalifu wa Wazayuni mwaka 1948, lakini leo niliona video ambayo ilibadilisha mtazamo wangu, ndani ya video hiyo, ilionesha wakati wa kufukuzwa kwa familia mbili za Kipalestina wakazi wa Quds; nyumba ambayo ilikuwa urithi wa vizazi vingi vya mababu zao, wazayuni waliwalazimisha kuondoka nyumbani kwao ili badala ya familia hii asilia ambayo kwa maelfu ya miaka ilikuwa ikiishi katika mji huu mtakatifu, walete familia ya Kiyahudi isiyo na mizizi kutoka Amerika ya Kusini au Ulaya na kuiweka katika mji wa kale wa Quds.”

Nakba imeanza miaka 78 iliyopita na haijasimama hata kwa siku moja, kwa miaka 78 wamekuwa wakijaribu kutuangamiza sisi Wapalestina, wameharibu vijiji, miji na miti, wamemuangamiza Mpalestina, lakini hawajawahi kufikia lengo lao, Kila wanapokwenda, mawe na miti iliyochoka ya ardhi hii hupaza sauti kutangaza kuwa ni ya Kipalestina, Palestina bado iko hai katika nyoyo na akili zetu sisi watu wanaodhulumiwa.

Kila siku mamia ya familia katika Ukingo wa Magharibi, Quds na kusini mwa Palestina inayokaliwa kwa mabavu (Naqab) hulazimishwa kutoka katika nyumba zao, hulipa faini nzito na kufanywa wakimbizi.

Sasa tumebaki sisi; kizazi cha tatu cha Nakba, sisi ambao huko Quds tunatoa mashahidi, huko Ghaza nyumba zetu zinapigwa mabomu, huko Ukingo wa Magharibi ardhi zetu zinataifishwa; sisi ambao kila siku tunaigusa Nakba kwa nyama na ngozi yetu; sisi tulikuwa kizazi ambacho kwa mara ya kwanza katika operesheni ya Tufani ya Al-Aqsa tuliweza kuingia katika ardhi zetu zinazokaliwa kwa mabavu na kuwapa wapokonyaji mapigo makali na yenye maumivu; kizazi ambacho kinaamini katika ukombozi wa karibu wa Palestina na kitapigana kwa ajili ya lengo hili hadi tone la mwisho la damu.

Licha ya kuendelea kwa uhalifu wa utawala wa Kizayuni nchini Palestina, kutolewa hukumu za kunyongwa kwa wafungwa bila mashitaka na hukumu ya haki, ukimbizi na mashambulizi ya mfululizo dhidi ya watu waliodhulumiwa wa Palestina, swali linalojitokeza akilini ni kwamba; baada ya kupita karibu miaka mitatu tangu kuanza kwa operesheni ya Tufani ya Al-Aqsa, je, Umma wa Kiislamu unapaswa kusubiri kuendelea kwa uhalifu huu au kuanza kwa tufani nyingine ambayo itaung’oa mizizi yake, ambao katika vita vya hivi karibuni dhidi ya Iran umeonekana dhaifu zaidi kuliko wakati mwingine wowote?

Lebo

Maoni yako

You are replying to: .
captcha